» »Unlabelled » Mbaroni kwa kudaiwa kuua mwenzake

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji


JESHI la Polisi, Mkoa wa Ruvuma, linamshikilia Yazidu Abina (35), mkazi wa Kijiji cha Mrusha, Wilaya ya Tunduru, mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua Rajabu Mohamed (45) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kichwani na machoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba mbili mwaka huu, usiku katika eneo la Pacha Nne.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwombeji, kabla ya tukio hilo, Rajabu Mohamed alituhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa mtuhumiwa Abina.

“Inasemakana siku ya tukio, mtuhumiwa Abina akiwa shambani, alichukua kitu chenye ncha kali na kumvizia marehemu Rajabu Mohamedi na kumchoma kichwani na machoni kwa kutumia kitu hicho na kumuua,” alisema Kamanda Mwombeji.

Kutokana na tukio hilo, kamanda huyo wa polisi amewataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kuachana na tabia za kujichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

“Waambieni wananchi wasiwe na utaratibu wa kujichukulia sheria mkononi kwani huyo aliyemuua mwenzake tutamfikisha mahakamani wakati wowote ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema.

Katika tukio jingine, Kamanda Mwombeji alisema wanawashikilia watu 17 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio mbalimbali ikiwamo wizi wa kuvunja nyumba.

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na mali za watu ambazo zilitambuliwa na wamiliki wake baada ya kuwapo kwa taarifa za watu hao kukamatwa.
Alizitaja baadhi ya mali zilizokamatwa kuwa ni compyuta mpakato sita, compyuta za mezani, televisheni 18, redio na vifaa mbalimbali vya pikipiki.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post