» »Unlabelled » Hutoisikia tena kazi ya Avril na Darassa, hii ndio sababu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Darassa na Avril wakiwa kwenye studio za Wanene Ent

Hutosikia tena kolabo kati ya msanii wa Kenya, Avril na rapper wa Bongo, Darassa, kwanini? Ngoma hiyo ipo kifungoni, walau kwa mujibu wa maneno ya Darassa mwenyewe.

“Hiyo project na Avril, ni moja kati ya project ambazo zipo kifungoni tunasema. Hatuwezi kuirelease sababu hatutaki kuingilia taratibu za watu wala watu waingilie taratibu zetu. Project ya Avril haitatoka sababu tulirekodi kwenye studio ambayo tulikuja kutokea tafrani kidogo ya maelewano,” Darassa alimuambia Natty E wa Jembe FM.

 Avril akiwa na Hanscana kwenye studio za Wanene. Muongozaji huyo hafanyi tena kazi na kampuni hiyo

Wimbo huo ulirekodiwa kwenye studio za Wanene Entertainment, wiki 8 zilizopita. Tafrani gani hiyo anayoisema Darassa iliyopelekea kazi yake kutiwa kifunguni? Huenda Hanscana akawa anahusika.
 Darassa akiwa kwenye studio za Wanene Entertaiment na engineer wa studio hizo (aliyekaa), Avril na producer Abbah Process

Wimbo huo ulirekodiwa wakati Hanscana, swahiba wa Darassa alikuwa bado mfanyakazi wa Wanene Entertainment. Baada ya muongozaji huyo kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo, kazi zake zote alizozifanya mikononi mwao, zilipigwa kufuli – ikiwemo kazi ya mwanae Darassa!
Darassa na Avril wakipongezana kwa kazi nzuri ambayo hata hivyo ipo kifungoni na haiwezi kuja kuuona mwanga wa siku tena

Inasikitisha kwasababu Avril alivutiwa na kazi hiyo. “Class is in session! Really amazing getting a chance to hang out/work with @darassacmg and producer @abbah_process,” aliandika kwenye Instagram.

Darassa anabaki na option nyingine – kumleta tena Avril Bongo, kwenda kwenye studio nyingi na kumalizia walichokianza.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post