» »Unlabelled » Chura wa Snura aachiwa huru baada ya kufanyiwa marekebisho

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO



Snura akizungumza na waandishi wa habari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemruhusu msanii wa muziki, Snura Anthony Mushi ‘Snura’ kuachia video yake mpya ya wimbo ‘Chura’ baada ya msanii huyo kufanya marekebisho ya video ya wimbo huo na kukubaliwa na wizara.

Aidha, katika barua ya wizara imemtaka Snura kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari ili video hiyo ianze kuchezwa.

Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar es salaam, Snura amesema anamshukuru Mh waziri Nape Moses Nnauye kwa kumkubalia ombi lake la kuiruhusu kazi hiyo kutoka.

“Mh Nape ameuruhusu wimbo wangu mpya wa Chura na video Chura kupigwa na kuonyeshwa katika vituo mbali mbali vya radio na runinga baada ya kuona video yangu mpya ya wimbo ina maadili na ujumbe ndani yake ikiwa ni kukidhi makubaliano ya awali kwamba wimbo wangu ‘Chura’ utakafunguliwa pale nitakapofanya video mpya ya muziki yenye maadili ya kitanzania,” alisema Snura.

Aliongeza, “Video yangu mpya Chura inaeleza maana halisi ya neno Chura. Chura ninae mzungumzia ni mwanamke anaeruka ruka katika mahusiano kwa kubadilisha wanaume mbalimbali matokeo yake kupata magonjwa sugu,”.

Pia katika barua hiyo ya Mh Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempa onyo kali msanii huyo kutokurudia kufanya tena video zisiyokuwa na maadili ya kitanzania.

Barua ya wizara

Source: Bongo5
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post