
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (Kushoto),akimsalimia mmoja ya wazee walio katika kituo cha kulelea wazee.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amesema kuwa serikali itashirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wazee na watu wenye ulemavu wanapata huduma za kijamii haraka iwezekanavyo.
Aidha amewaomba watumishi wa kituo hicho kukitumia vizuri chakula hicho, kutokana na viongozi wengine ambao ni watumishi wa vituo kama hicho, kutokuwa waadilifu, kutokana na kuuza chakula cha msaada unaotolewa kwa ajili ya kuwasaidia wazee wenye uhitaji.
Hata hivyo amewashukuru wadau mbambali ambao wamejitolea, kuwachangia wazee hao, huku akiziomba taasisi za serikali, mashirika ya watu binafsi, na watu wote wenye mapenzi mema kujitahidi kuwasaidia wazee.
