
Baraza la taifa na uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini (NEMC) limeitoza faini ya shilingi milioni 12, halmashauri ya manispaa ya Tabora, kutokana na kutoweka mundombinu ya kukusanya taka ngumu, kuziacha eneo la shughuli za watu kwa mda wa zaidi ya mwezi mmoja, hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Hatua hiyo ya kuitoza faini manispaa ya Tabora imetokana na ziara ya kushitukiza naibu waziri ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira, Mhe. Luhaga Jackson Mpina, aliyoifanya katika soko kuu la mjini Tabora, na kubaini taka ngumu zamda mlefu, ambapo amepokea malalamiko ya wafanyabiashara wakidai kuwa, uongozi wa manispaa umewatelekeza.
Akizungumza na wafanyabiashara hao mara baada ya kumuhoji mkurugenzi wa manispaa hiyo, Bw, Bosco Ndunguru, ambaye amekiri kuwepo na changamoto ya ukusanyaji taka, Mhe, Luhaga Mpina, amesema, serikali haitawavumilia watendaji ambao hawatimizi wajibu wao kwa wananchi.
Akitoa adhabu hiyo ambayo imedaiwa kuwa ni ya kwanza NEMC kuiwajibisha halmashauri, afisa mazingira mwandamizi, Bw Benjamini Doto amesema kuwa, baraza limefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha juu ya uzembe wa uzoajo taka ngmu wakati ni wajibu wa halmashauri kuweka mikakati ya kufanya usafi maeneo ya biashara.
