» »Unlabelled » Hiki ndio kipaumbele cha kwanza kwa katibu mkuu mpya UN

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Katibu Mkuu Mteule wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kipaumbele chake cha kwanza ni kushughulikia ukosefu wa amani duniani ambao amesema ndiyo changamoto kubwa hivi sasa.
Amesema hayo wakati akizungumza kwa mara ya kwanza kabisa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya kupitishwa na Baraza Kuu.
Bwana Guterres, amesema mizozo ya zamani imeendelea kuwepo, mipya ikiibuka huku ukwepaji sheria ukizidi kushamiri hivyo na kusema kuwa ongezeko la matumizi ya diplomasia katika kusaka amani itakuwa kipaumbele changu.
Aidha Bw. Guterres amesema kuna changamoto kubwa kuhusiana na marekebisho ya chombo hiki kiweze kuwa na ufanisi na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa watu tunaowahudumia 

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post