
Shirika la ndege nchini ATCL limekamilisha taratibu zote za kuziwezesha ndege zake mbili mpya zilizonunuliwa hivi karibuni kuanza kutoa huduma katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Wakizungumza baada ya moja ya ndege hizo mpya aina ya Bomberdier Q400 Nextgen kutua katika uwanja wa ndenge wa Arusha ikiwa ni safari ya majaribio mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa shirika hilo Bw Ibrahimu Musa amesema ndege hizo zitaanza safari wakati wowote kuanzia sasa.

Bw Ibrahim amesema taratibu za kitaifa na kimataifa zimekamilika na kwamba kwa kianzia ndege hizo zitaanza kutoa huduma hapa nchini na baadaye zitaanza safari za kwenda nchi mbalimbali ikiwemo Komoro.
Kwa upande wake Mhandisi wa shirika hilo ambaye pia ni mtaalam wa usalama wa anga Bw John Chaggu amesema wameshafanya ukaguzi katika viwanja vyote vya ndege katika mikoa ambayo ndege hizo zitatoa huduma na baadhi ya mapungufu yaliyokuwepo katika baadhi ya viwanja kikiwemo cha kigoma zimesharekebishwa.
Kwa mujibu wa Mhandisi huyo tayari ndege hizo zimeshafanya safari za majaribio katia viwanja vyote zitakazotoa huduma.
