» »Unlabelled » Makamba aagiza watu kuondolewa mara moja katika chanzo cha maji Morogoro

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Morogoro.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, January Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, John Mgalula kuhakikisha kuwa ifikapo Novemba 30 mwaka huu watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu katika chanzo cha maji cha Mambogo waondolewe haraka.

Waziri Makamba alitoa agizo hilo leo wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Mambogo kinachotegemewa na wananchi wa Manispaa ya Morogoro mara baada ya kujionea uhalibifu unaoendelea kufanywa na wananchi hao na kusababisha maji kukauka.

Waziri huyo alimtaka mkurugenzi huyo kuwaondoa na kuwafikisha mahakamani wale wote waliochepusha maji kutoka katika chanzo hicho kwani wamekuwa wkaifanya hivyo kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo zinazokataza kufanyika kwa shughuli zozote za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post