Kibiti. Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Mariam Haji mkazi wa Kitongoji cha Mbebetini wilayani Kibiti mkoani Pwani kwa tuhuma za kumnyonga mwanaye hadi kufa kisha kuutupa mwili wa marehemu kwenye kisima chenye maji.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventure Mushongi alisema mwanamke huyo alitumia kamba ya kitambaa kumnyonga mwanaye Majaliwa Muhidini mwenye mwezi mmoja hadi kufa.
Alisema mwanamke huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo alikwenda kuutupa mwili wa mtoto huyo kwenye kisima cha maji.
Alisema kutokana na tukio hilo jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi dhidi ya tukio hilo.