Moshi. Dereva wa lori aina ya Mitsubish Fusso na utingo wake wamefikishwa mahakamani wakidaiwa kusafirisha kilo 346.58 za dawa za kulevya aina ya mirungi.
Waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Pamela Meena ni dereva Ally Msangi (26), utingo Rashid Salim (22) na Hamza Juma (22) ambaye ni mkulima.
Wakili wa Serikali, Agatha Pima, akiwasomea mashtaka alidai Septemba 28, katika barabara ya Holili-Himo walisafirisha dawa hizo.
Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo bali Mahakama Kuu. Kesi imepangwa kutajwa Oktoba 25.
Kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2015, shtaka linalowakabili washtakiwa hao halina dhamana kama ilivyo kwa makosa ya mauaji, wizi wa kutumia silaha na uhaini.