» »Unlabelled » Rais Buhari wa Nigeria apewa Onyo na Mkewe

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Muhammadu Buhari. Picha: Septemba 2016Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionRais Muhammadu Buhari aliahidi kukabiliana na ufisadi serikalini

Mke wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ameonya kuwa huenda asimuunge mkono mumewe kwenye uchaguzi mkuu ujao iwapo kiongozi huyo hatafanya mabadiliko kwenye serikali yake.
Kwenye mahojiano na BBC, Aisha Buhari amesema rais huyo "hawafahamu" wengi wa maafisa wakuu aliowateua serikalini.
Amedokeza kwamba serikali imetekwa, na kwamba kuna "watu wachache" ambao huamua ni nani watateuliwa au kupewa kazi na rais.
Bw Buhari alichaguliwa mwaka jana baada yake kuahidi kukabiliana na ufisadi uliokuwa umekithiri serikali pamoja na ubaguzi na mapendeleo.
Uamuzi wa mke wa kiongozi huyo kusema hayo hadharani umeshangaza wengi, lakini ni ishara ya kiwango cha kutoridhishwa kwa watu na uongozi wa Rais Buhari, anasema mwandishi wa BBC aliyepo Abuja, Naziru Mikailu.
Rais Buhari alitangaza wakati wa kuapishwa kwake kwamba yeye "hamilikiwi na mtu yeyote na anamilikiwa na watu wote".
Kwenye mahojiano na Naziru Mikailu, Bi Buhari alisema: "Rais hawafahamu 45 kati ya 50, kwa mfano, kati ya watu aliowateua na mimi mwenyewe siwafahamu, licha ya kwamba nimekuwa mke wake kwa miaka 27."
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post