» »Unlabelled » Yanga yapeleka Azam Fc Shinyanga

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


AZAM FC imeamua kuweka kambi Shinyanga kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Oktoba 16 mjini Dar es Salaam.


Uamuzi huo unakuja siku moja baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wake dhidi ya wenyeji, Stand United jana Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kwa kufungwa 1-0.



Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi alisema jana katika mazungumzo na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba timu itabaki Shinyanga kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga Jumapili.Tokeo la picha la azam fc


Azam FC imeweka kambi Shinyanga kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga SC Oktoba 16 

Alisema kwamba benchi la Ufundi na wahezaji wamekubaliana na matokeo ya jana na sasa wanajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Yanga ili warejeshe heshima.



“Kwa kweli hali ilivyo inasikitikisha, ila hatujakata tamaa. Tunaendelea kupambana na sasa tunajipanga kwa mchezo ujao,”alisema Iddi.



Azam FC, washindi wa pili wa msimu uliopita Ligi Kuu – mambo si mazuri msimu huu baada ya kuambulia pointi 11 katika mechi nane, wakishinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili hivyo kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi. 
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post