» »Unlabelled » Utajiri wa Serena Williams ni balaa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

MWANDISHI WETU na Mitandao
AKIWA Amezaliwa Septemba 26 mwaka 1981, Serena Williams, mchezaji bora wa muda wote wa mpira wa wavu maarufu kama Tennis, ana utajiri mkubwa unaofi kia kiasi cha dola milioni 145, sawa na shilingi bilioni 290.
 Ni mkwanja mrefu kwa Watanzania wengi, lakini cha kushangaza, binti huyo mwenye umri wa miaka 34 mwenye uwezo wa kupata kila anachokihitaji maishani mwake, hana mume, mtoto wala mchumba na kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe, vitu hivyo havipo kabisa akilini mwake kwa sasa! Mmarekani huyu mweusi mfuasi wa Shahidi wa Jehova, aliyezaliwa Saginaw, Michigan kutoka kwa wazazi Richard Williams na Oracene Price ni bingwa mara 15 wa michuano mikubwa ya tennis duniani na katika utajiri wake huo, dola milioni 67 amezipata kama zawadi kutokana na kushinda mashindano mbalimbali.
 Serena alianza harakati za kucheza mchezo huo akiwa na umri wa miaka 14 na alipofi kisha 17, akatwaa taji lake la kwanza. Hivi sasa, mkali huyo ambaye pia mdogo wake, Venus Williams naye ni mtoto wa kuotea mbali katika mchezo huo, anaingiza mkwanja kiasi cha dola 98,400 kwa siku, sawa na shilingi 206, 640,000!

Ingawa mchezo wa Tennis ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya Serena, lakini pia msichana huyu anaingiza fedha kupitia dili mbalimbali anazopata kutoka kampuni kubwa zikiwemo za michezo, kama ilivyo kwa Nike, ambayo iliingia naye mkataba uliomfanya aweke kibindoni kiasi cha dola milioni 40!

Mwanamichezo huyu pia anaingiza ‘mpunga’ kupitia mikataba yake na Kampuni za Wilson, JP Morgan Chase, Kraft Foods, Gatorade, OPI na Berlei Bras. Kwa pamoja kampuni hizi zinamuingizia dola milioni 12 kwa mwaka!

Shirikisho la mchezo huo duniani, WTA limemtangaza mara nyingi kuwa mchezaji namba moja kwa ubora, baada ya kuwa ameshashinda mataji 68 ya peke yake, 22 ya wawili wawili na mawili ya zaidi ya wawili.
 Serena anamiliki mjengo wa hatari huko West Palm Beach, katika eneo la ‘wenye nazo’ la Ballen Isles, Florida lenye thamani ya dola milioni 2 sawa na madafu bilioni 4.2, ambao ndani yake kuna viwanja vya mchezo wa Tennis vipatavyo 22. Pia lina vyumba vitano vya kulala, mabafu manne na bwawa la kuogelea.

Chumba chake cha kulala kimenakshiwa kwa madini ya bei mbaya, bila kusahau uwepo wa maktaba kubwa inayomfanya wakati mwingine akae siku nzima akijisomea bila kutoka nje. Analo pia eneo la makumbusho lililojaa medali za harakati zake zote za Tennis.

Uwepo huo wa viwanja ndani ya eneo lake, umemfanya asiwe na mwendo mrefu kuelekea mazoezini na pia kuwafanya wachezaji wenzake nao kuvutika kuelekea Ballen Isles ambao ni Aaron Krickstein na Ivan Lendi Katika eneo lake la kuegeshea magari, Serena amejaza magari ya kifahari, likiwemo Bentley Supersports lenye thamani ya dola 321,100 ambazo ni sawa na shilingi milioni 674!
Pia Serena Williams analo gari aina ya Bently lenye thamani ya dola 120,000, achilia mbali boti za kifahari ambazo huzitumia kwa kujipumzisha na wanafamilia wake wengine.

Kipato hicho kinamfanya mwanamichezo huyo kutajwa kuwa ndiye mwenye mkwanja mrefu zaidi kuliko wanamichezo wote wa kike duniani kwa sasa.

Serena Williams Net Worth

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post