» »Unlabelled » Raia wawili wa kigeni wakamatwa wakiwa watumishi wa Serikali

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

RAIA wawili wa Kigeni wakamatwa jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuishi hapa nchini bila kibali na kuwa watumishi wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule amesema kuwa  Raia hao ni Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo  na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi.

Amesema kuwa Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kinyume na sheria za nchi, na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa Tanzania.
Watuhumiwa ambao sio raia wa Tanzania waliokuwa wakifanya kazi serikalini wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa Uhamiaji, kushoto ni Bw. Bahilanya Milingita aliyekuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)na kulia ni Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya Mburahati.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post