» »Unlabelled » Dully Sykes asema WCB wamegharamia video ya Inde

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mkongwe Dully Sykes alishikwa mkono na kijana wa WCB, Harmonize ambaye label yake iligharamikia kila kitu kwenye mradi wake mpya, Inde.

Akiongea na Clouds E ya Clouds TV, Dully alidai kuwa Inde ni zawadi aliyopewa na WCB kama kumlipa fadhila ya jinsi alivyokuwa msaada mkubwa kwa Diamond na wasanii wengine wa label hiyo. Amedai kuwa hakuwa na mpango wa kuachia ngoma mpya hadi mwakani.

Staa huyo ameongeza kuwa pamoja na kuwa ni producer na mmiliki wa studio yake mwenyewe, aliamua kuacha Inde ifanywe kwenye studio za WCB ili kupata ladha mpya.

Hata hivyo aliongeza kuwa ni yeye ndiye alimpa wazo Diamond la kuanzisha studio yake mwenyewe na kwamba anafurahi kuona kuwa wazo hilo lilifanyiwa kazi na limezaa matunda.


ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post