» » Watumishi 3600 hatihati kukosa mishahara Pwani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki

Pwani.  Uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mkoani Pwani kuwaweka watumishi 3,600 kwenye hatari ya kukosa mishahara ya Agosti mwaka huu baada ya kubaini mapungufu katika taarifa zao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki  amesema kati ya hao, watumishi 3,569 taarifa zao za kielimu hazionekani,36 wana zaidi ya miaka 60 lakini wako kazini badala ya wamestaafu, sita akaunti zao hazitambuliki na 21 vyeo vyao havijabainishwa.

Amesema hivyo haitawezekana kulipwa mishahara kuanzia Agosti hadi hapo mapungufu ya taarifa zao zitakaporekebishwa.

Akizungumza na watumishi wa umma Pwani, Kairuki amesema Bagamoyo ina watumishi 2,175 wenye taarifa zenye upungufu, Rufiji (912), Kibaha Mji(465), Mkuranga (21) Kibaha Vijijini (14), Mafia na Kisarawe (8).
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post