pesa ya nauli ya daladala lakini AY alimtia nguvu na faraja na kusema itafika wakati watafanikiwa na kufurahia mafanikio yao.
Mwana FA anasema kuwa kila anapokutana na magumu yoyote huwa anakumbuka kauli hiyo ya AY na kumkumbusha na kudai kamwe hawezi kuisahau kauli hiyo aliyoitoa AY kati ya mwaka 2003 au 2004.
"Kuna siku mwaka aidha 2003 ama 2004, hatuna hata nauli ya daladala ya kwendea mjini, huyu jamaa (AY) akaniambia "easy mwanangu, utafika wakati tutakuwa tunaazimana magari" Kama kauli ndogo tu hivi eeehh? well, sijawahi kuisahau na huwa namkumbusha kila wakati tunapopata ugumu kwenye mambo yetu. Jifunze kitu. Mungu akulinde uendelee ku'spread positive vibes only". Aliandika Mwana FA
