» » Serikali kuwakamata wanaowaficha wahamiaji haramu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Kutokana na tatizo la wahamiaji haramu kuendelea kuingia nchini na kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Kutokana na tatizo la wahamiaji haramu kuendelea kuingia nchini na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, serikali imeanza kudhibiti vitendo hivyo kwa kuongeza ulinzi maeneo ya mipakani.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na East Africa Radio kuhusu kuongezeka kwa wimbi la wahamiaji haramu nchini ambapo washiriki wakuu wanaowasaidia wahamiaji hao kuingia nchini ni baadhi ya watanzania ambao si waaminifu wanawaingiza wahamiaji hao na kuwahifandhi kwenye majumba yao kinyume cha sheria ya nchi inavyoelekeza.

Amesema serikali imeanza kuwadhibiti wahamiaji hao haramu kwa kuanzia oparesheni maalumu yakuwakamata watu hao na kuwafungulia mashtaka sambamba na kuwarudisha makwao.

Amesema kwa sasa wameamua kuanza kuwashirikisha viongozi wa serikali za vijiji katika kupambana na jambo hili ambalo kama litaachiwa bila kushughulikiwa kwa wakati litasababisha matatizo makubwa hasa kwa siku za mbeleni.

Amesema jukumu la ulinzi na usalama nchini ni jukumu la kila Mtanzania na kila mmoja ashiriki kupiga vita vitendo hivyo vya kikatili.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post