Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wales Chriss Coleman amesema licha ya kutopewa nafasi kubwa ya kushinda leo dhidi ya Ureno lakini wao wamejipanga kikamilifu katika mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ya mataifa bingwa Ulaya.
Coleman amesema aina ya mchezo na utamaduni wao ni vitu viwili vyote kwa pamoja vimewaunganisha na ana imani umoja uliopo ndani ya timu wataweza kufanya makubwa katika michuano hii.
Kocha huyo ameiongoza kwa mara ya kwanza Wales kutinga nusu fainali ya mashindano makubwa tangu mwaka 1958.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Soka cha Wales Jonathan Ford amesema wananchi wote nchini mwao wamewatakia kila la kheri wachezaji wao ili waweze kuifanya ndoto yao kuwa kweli msimu huu.