» » Klabu ya AC Milan imeuzwa kwa Wachina

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Aliyekua Waziri Mkuu wa Italia na mmiliki wa klabu ya Ac Milan, Silvio Berlusconi amethibitishwa kuuzwa kwa klabu hiyo kwa wawekezaji kutoka nchini China.

Berlusconi ametamka kuwa wawekezaji hao watakua wakilipa angalau paundi milioni 220 kwa miaka miwili ijayo itakayoifanya klabu kuwa na thamani ya Euro milioni 750 ikijumuisha na madeni iliyonayo.

Ingawa mmiliki huyo ajataja jina la kampuni la wawekezaji hao lakini inaaminika kuwa watakua wakimiliki asilimia themanini ya hisa zote za klabu hiyo yenye historia kubwa katika mashindano mbalimbali barani Ulaya.

Inaaminika kua ujio wa wawekezaji hao utaifanya Ac Milan kuwa na uwezo wa kupambana na wapinzani katika soko la usajili na mambo mengine ya kiushindani na kuiwezesha kurejesha heshima yake iliyojiwekea miaka mingi iliyopita.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post