» » » Ciara anahofia Future anaweza kumuua mchumba wake, Russell Wilson

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Ciara anahofia kuwa ex wake rapper Future anaweza siku moja kuja kumuua mchumba wake wa sasa, Russell Wilson.

Hiyo ni kwa mujibu wa nyaraka za mahakamani ambazo muimbaji huyo aliwasilisha katika kesi yake ya kuchafuliwa dhidi ya baba huyo wa mwanae.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ , Ciara anadai kuwa kuna siku  Future alipost emoji za mpira huku akiweka emoji za bunduki kuzielekeza kwenye mipira hiyo kwenye Instagram.

Wilson, ni mchezaji wa timu ya football ya Seattle Seahawks.
Ciara pia alielezea wimbo wa Future, ‘Juice’ ambamo rapper huyo anasikika akizungumzia kesi za mauaji na ‘O.J. Simpson’. “Tryin’ to f**k my baby mama, dog what’s up with you?” You gon’ make me get that heat, I’m pulling up on you,” anarap Future.

Muimbaji huyo anaelezea kuwa vitendo hivyo vinatisha na kuelezea kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji ya bunduki.

Hata hivyo kufuatia taarifa hiyo, Future ametweet: Wish everyone could move on like me… that’s my only wish.”

February, Ciara alifungua kesi ya dola milioni 15 dhidi ya Future kwa madai amemchafua. Future naye alifungua yake April lakini aliifuta mwezi uliopita.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post