» » Taylor Swift kuwashitaki Kanye, Kim

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


                                                        Taylor Swift

Mwanamuziki Taylor Swift yuko mbioni kuwashitaki wanandoa Kim Kardashian na Kanye West kufuatia kuvuja kwa mazungumzo ya siri yaliyofanyika kati ya Taylor na Kanye.

Taylor anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za California ambapo kurekodi mazungumzo bila kukubaliana kisha kuyavujisha ni kosa kisheria.


                                                 Kim Kardashian na Kanye.

Inadaiwa kuwa, awali Kanye na Taylor walifanya mazungumzo ambapo Kanye alitaka amuite Taylor malaya kwenye wimbo wake mpya wa Femous lakini Kim akayanasa na kuyaanika mtandaoni.

Inaelezwa kuwa, baada ya mazungumzo yao kuwekwa hadharani, Taylor alikasirika sana na ana mpango wa kuwashitaki wanandoa hao na tayari amelifikisha suala hilo kwa mwanasheria wake.

Kufuatia saga hilo, wapo waliodhani Kanye atakinukisha kwa Kim lakini katika siku za hivi karibuni wanandoa hao walionekana wakiwa na furaha kama vile hakuna lililotokea.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post