Sauti iliyorikodiwa kutoka chumba cha rubani cha ndege ya Misri
iliyoanguka katika bahari ya Mediterania mwezi Mei, zinaashiria
kufanyika kwa juhudi za kujaribu kuuzima moto uliowaka ndani ya ndege
hiyo.
Vyanzo vya habari kutoka kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo, vimesema sauti hizo zinakwenda sambamba na rekodi za ndani ya ndege hiyo, ambazo awali zilidokeza kwamba moshi ulifuka katika chumba cha kuongozea ndege, na katika vyoo vya ndege hiyo.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Misri, EgyptAir chapa MS804 ilianguka baharini tarehe 19 Mei ikiwa safarini kutoka Paris kwenda Cairo, na kuuwa watu wote 66 waliokuwa ndani yake.