Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema kuwa kati ya Halmashauri saba
za mkoa huo, halmashauri ya jiji pekee ndio haijakamilisha zoezi la
utengenezaji wa Madawati licha ya kwamba tarehe ya kikomo imepita.
Akizungumza wakati akipokea msaada wa Madati 400 kutoka kwa Kampuni ya
uchimbaji wa Madini ya Panda hili Tanzania Limited ambayo inatarajia
kuanza kuchimba Madini adimu Duniani aina ya NIOBIUM, amesema Wilaya ya
Mbeya ni miongoni mwa halmashauri sita zilizokamilisha zoezi la
utengenezaji wa madawati.
Makala amesema kuwa jiji la Mbeya limeshindwa kukamilisha zoezi hilo kwa
muda uliopangwa kwa sababu lilielekeza tenda kwa chuo cha Ufundi VETA
pekee.
Makala amesema halmashauri hizo zina ziada ya Madawati na kwamba jiji la
Mbeya kwa kushirikiana na ofisi yake wamehamisha Tenda kwa mtu Mwingine
ambaye atafanya zoezi hilo kwa muda mfupi.