Kipa namba moja wa Simba, Vincent Angban raia wa Ivory Coast, amerejea
nchini na umeungana na kikosi chake kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi
ya msimu ujao wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Angban alitakiwa kutua nchini Jumapili iliyopita akiambatana na mshambuliaji raia mwenzake wa Ivory Coast ambaye anatarajiwa kusajiliwa na Simba, Blagnon Goue Fredric, lakini alishindwa kufanya hivyo baada ya kudaiwa kuchelewa ndege.
Hata hivyo, Fredric ambaye ni mshambuliaji yeye alitua peke yake siku hiyo ya Jumapili na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo ambao tayari wanadaiwa kufanya naye mazungumzo ya awali na kinachosubiriwa sasa ni kuangaliwa uwezo wake na Omog ndipo aweze kusajiliwa.
Meneja wa Simba Abassi Ally alisema kuwa Angban ametua juzi Jumatatu na kwenda moja kwa moja kuonana na viongozi wa timu hiyo.