» » Sababu za Jeshi la Polisi kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Jeshi la polisi nchini limeendelea kusisitiza msimamo wake wa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa mpaka hapo hali ya usalama itakapotengemaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kamishina wa polisi operesheni na mafunzo makao makuu ya jeshi la polisi nchini Nsato Mssanzya amesema jeshi la polisi halitakubaliana na kauli za uchochezi zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa ambazo  zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani kwa jamii.

Kamishna Mssanzya amesema jeshi la polisi litaendelea kuimarisha hali ya usalama kwa wananchi wake ikiwemo kulinda usalama wa raia na mali zao huku likiwataka baadhi ya wanasiasa kufuata sheria na taratibu ambazo zimewekwa .

Mssanzya amesema jeshi la polisi limepiga marufuku maandamano pamoja na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa huku likifafanua kuwa jeshi hilo halitaingilia mikutano ya ndani inayofanywa na vyama hivyo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post