» » Uhaba wa Mafuta Mtwara watumiaji wagombaniana

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya diesel na petrol mkoani Mtwara wamefikia hatua ya kupata mafuta kwa kugombana kwenye kituo cha mafuta kufutia na uhaba wa bidhaa ambapo kituo kimoja pekee cha mafuta kati ya vilivyopo katika manispaa ya Mtwara Mikindani kinauza mafuta huku vikingune vikiwa havitoi huduma hiyo.

Hali hiyo imeanza tangu mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA kutangaza kupanda kwa bei ya mafuta kulingana na soko la dunia.

Mwandishi wetu Adam Malima kutoka mkoani Mtwara anayo taarifa zaidiÖ..

Ni sheli moja ya Total inayotoa mafuta kati ya sheli nane zilizopo hapa manispaa ya Mtwara mikindani na upataji wake wa mafuta ni wakugombana.

Watumiaji wa mafuta wameeleza kukerwa na upangaji wa foleni kwa mda mrefu wakisubiri kujaza mafuta katika kituo kimoja ambapo napo wapo mguu upande kwa maana mda wowote wanaweza kuondoka bila kupata mafuta.

Moja kati ya wahusika wa sheli ya mafuta ya Total inayotoa huduma,Salma Shaibu amesema tatizo hilo linaanzia Dar es Salaam wanakochukulia mafuta.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post