Mkufunzi Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kuchukua jukumu la
kuifunza Manchester United,akisisitiza ''niko mahala nitakapo''.
Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ''Nadhani ni kazi
ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi
nimeipata''.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea anachukua mahala pake Louis Van
Gaal,ambaye alifutwa kazi baada ya United kushinda kombe la FA mnamo
mwezi Mei.
Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki
katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini
akasisiiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji.
Nataka kila kitu,alisema.Nataka kushinda mechi,nataka kucheza vizuri sitaki kufungwa magoli.nataka mashabiki kutuunga mkono.

