» » Dodoma nini, mambo Dar bwana!

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dar es Salaam. Siku zote Dar es Salaam ndiyo kila kitu. Ni jiji la maraha. Hivi ndivyo  ilivyodhihirika kwa timu za Mwadui, Ndanda na Mtibwa Sugar zilipokimbia mikoa yao na kuweka kambi zao kwa maandalizi ya msimu ujao.

Timu hizo tatu zimepiga kambi zao kwa wiki kadhaa zikijiandaa kwa Ligi Kuu itakayoanza Agosti 20; Ndanda itaanza msimu mpya na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mtibwa Sugar itawakaribisha maafande waliopanda daraja, Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro wakati Mwadui itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kucheza na Toto Africans.

Mwadui ndiyo ilianza kulivamia Jiji la Dar es Salaam na kuweka kambi na baadaye Mtibwa ikafuata na mwishoni mwa wiki Ndanda imetua nayo pia kuweka kambi ya muda.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post