» » WWF yatoa ndege nane kukabili ujangili nchini

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Dar es Salaam. Profesa Jumanne Maghembe ameiomba Jumuiya  ya Kimataifa, kuunga mkono juhudi za Serikali  kupiga vita ujangili kwa vitendo katika kuimarisha uhifadhi nchini.

Maghembe aliyasema hayo jana alipokuwa akipokea msaada wa ndege nane zisizo na rubani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili nchini, zilizotolewa na Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF).

Ndege hizo ndogo maarufu drones, zenye thamani ya Dola za Marekani 80,000 sawa na zaidi ya Sh172 milioni, zitatumika katika Hifadhi ya Selous kuimarisha ulinzi wa wanyama kwa kukusanya taarifa za kiintelijensia zitakazosaidia kukamatwa majangili.

Alisema changamoto inayoikabili hifadhi ya hiyo ni ujangili ambao umesababisha idadi ya wanyama, hasa tembo kupungua kwa kasi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

WWF hivi karibuni ilitoa ripoti kuwa hifadhi hiyo imepoteza asilimia tisini ya tembo wake na waliosalia wako hatarini kupotea kabisa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post