» » Wapanda bodaboda Dar kupewa kesi za ‘kujiua’

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema watu watakaopanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu watakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kutaka kujaribu kujiua.

Aidha, alisema mtu anayepanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu anamfananisha na mtu anayetaka kumeza vidonge vya klorokwini na pombe kali kwa madhumini ya kutaka kujiua.

Aliyasema hayo juzi jioni katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB kwa wateja wake.

Alisema tayari ameshawaagiza askari wa usalama barabarani kuwakamata waendesha pikipiki na abiria wasiovaa kofia ngumu.

“Nimeagiza trafiki wote kwenye mkoa wangu wawakamate na nitawashtaki kwa kosa la kujaribu kujiua,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alisema, atautumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kutangaza mambo matatu ambayo aliyataja kuwa ni kuongeza muda wa kufanya biashara hasa kwa maduka makubwa kwa kuwa watu wengi ni wafanyakazi hivyo hawana muda wa kufanya manunuzi.

Aidha, atautumia mwezi huu kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya mikusanyiko ya watu na pia anaangalia uwezekano wa kudhibiti uvutaji wa shisha.

“Watafiti wangu walikuwa na kazi moja na wameikamilisha, kuna kaugonjwa kapya kameingia kwenye mkoa wetu, kaugonjwa kenyewe ni uvutaji wa shisha, imefikia mahali vijana hawawezi kulala au kula bila kuvuta shisha, sasa hatuwezi kwenda hivyo,” alisema.

Aidha, Makonda aliaomba Waislamu wote kuliombea, taifa lakini pia kuwaombea viongozi ili waweze kuongoza kwa busara na hekima. Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema, wameandaa futari hiyo mahususi kwa wateja wao katika kufurahia pamoja mwezi mtukufu wa Ramadhani.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post