
Muheza.
Benki ya CRDB imetoa madawati 60 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, ikiwa ni kuunga mkono
juhudi za Rais John Magufuli kupambana na uhaba uliopo kwenye shule
mbalimbali hapa nchini.
Meneja wa CRDB Mkoa wa Tanga, Evarist Mnyele amemkabidhi rasmi madawati hayo Mkuu wa wilaya ya Muheza, Esteria Sekilasi.
Meneja wa CRDB Mkoa wa Tanga, Evarist Mnyele amemkabidhi rasmi madawati hayo Mkuu wa wilaya ya Muheza, Esteria Sekilasi.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Mnyele amesema wameamua kutoa msaada huo
ili kurudisha faida kwa wananchi kwa sababu benki hiyo imetokana nao,
hivyo kuna kila sababu ya kusaidia shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza
baada ya kupokea madawati hayo, Kilasi aliishukuru benki hiyo kwa kuona
umuhimu wa kusaidia kupunguza uhaba wa madawati wilayani humo na kwamba
yatasambazwa katika shule mbalimbali.
