Dar es Salaam. Baraza la Famasia Tanzania wamekamatwa dawa zenye thamani
ya Sh337 milioni baada ya kufanya operesheni ‘Safisha’ katika maduka ya
mikoa tisa nchini ambayo yalifunguliwa bila kufuata utaratibu.
Msajili wa baraza hilo, Elizabeth Shikalage amesema wanaofanya biashara ya dawa bila kufuata utaratibu wanavunja Sheria ya Famasia, Sura 311 pamoja na Sheria za nchi katika uendeshaji wa utoaji wa huduma za dawa.
Amesema walikagua maduka ya dawa 685, kati ya hayo, 432 yalifungiwa kutokana na ukiukwaji wa sheria ya uanzishaji na uendeshaji.
Amesema dawa zinazofaa kwa matumizi ya binadamu zina thamani ya Sh325 milioni na zisizofaa Sh11.2 milioni.