Dar es Salaam. Taasisi za fedha zimeandaa maonyesho kwa ajili ya kuzungumzia fursa mbalimbali za biashara, mipango ya uwekezaji na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Imori International, Leo Nyanduga alisema maonyesho hayo ya siku tatu yatazishirikisha taasisi za fedha na wananchi katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Nyanduga alisema taasisi hizo zitapata fursa ya kukaa pamoja na kujua jinsi ya kuzitatua changamoto zinazoikabili, ikiwamo kushirikisha wadau mbalimbali ili kuhakikisha uchumi unakua. Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Justina Joseph alisema asilimia ndogo ya Watanzania ndiyo wamekuwa wakitumia huduma za benki, lakini wanakosa elimu ya kutosha ya jinsi kutumia benki na uwekezaji katika soko la hisa. Maonyesho hayo yatahudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji pamoja na Mkuu wa Idara ya Malipo serikalini, Bernad Dadi.