» » SBL yakabidhi kisima cha maji Hanang

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Hanang. Zaidi ya wakazi 12,000 wa Katesh wilayani Hanang, mkoani Manyara wataondokana na kero ya maji baada ya kuchimbiwa kisima.

Kisima hicho kilikabidhiwa juzi na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Thobias Mwilapwa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha alisema kisima hicho kimegharimu Sh81 milioni na kwamba, ni mkakati wa kampuni hiyo kuisaidia jamii.

Wanyancha alisema mradi wa Katesh siyo tu kwamba utaboresha afya za wenyeji wa eneo husika, bali utaongeza uzalishaji mali hususan wanawake na watoto wa kike ambao hawatalazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji mbali.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mwilapwa alipongeza SBL kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia miradi ya jamii nchini.

“Licha ya kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa kupitia malipo ya kodi kwa wakati, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususan huduma za jamii,” alisema.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post