Las Vegas, Marekani. Mgombea mtarajiwa wa Chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump ameripotiwa kunusurika kuuawa baada ya kijana mmoja kujaribu kumpora ofisa wa usalama silaha yake.
Ripoti zinaeleza kuwa kuwa mwanamume mmoja raia wa Uingereza alijaribu kupora bunduki ya ofisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisiasa wa Trump, amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi mgombea huyo wa kiti cha urais.
Kwa mujibu wa hati za mashtaka, Michael Sandford (20) amesema kuwa aliendesha gari hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Trump aliyekuwa katika mkutano wa hadhara.
Tukio hilo linadaiwa kutokea mwishoni mwa wiki na tayari maofisa upelelezi wameanza kuchunguza mazingira halisi ya tukio lenyewe.
Imeelezwa kuwa, mtuhumiwa huyo alimfuata ofisa wa polisi na kuanza kumuuliza kitu, huku akitaka kupatiwa maelekezo kwa kuwa alitaka kuonana na Trump ili amsainie kitabu chake cha kumbukumbu.
“Sandford alimfuata ofisa huyo na kisha kuanza kuzungumza naye akitaka afahamishwe namna atakavyoweza kuonana na Trump kwa lengo la kusainiwa kitabu cha kumbukumbu.
Wakati wakiendelea na mazungumzo, Sandford kumpora ofisa huyo silaha yake,” ilieleza sehemu ya taarifa.
Hata hivyo, Sandford alidhibitiwa na kisha kuchukuliwa hadi hoteli moja ambako aliwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa zaidi.
Ripoti zilizotolewa baadaye na idara ya polisi zilisema kuwa kijana huyo alikuwa amepanga kumuua mgombea huyo tangu mwaka jana, lakini haikuelezwa sababu za kutaka kufanya hivyo.
Kabla ya kufanya tukio hilo inasemekana kuwa kijana huyo alikuwa amejifunza kulenga shabaha na kwamba amekuwa akiishi Marekani kinyume cha sheria kwa zaidi ya miezi 18.
“Alitueleza kuwa kabla ya kuja kwenye mkutano wa Trump, siku moja kabla alikuwa amejifunza kulenga shabaha,” alieleza ofisa wa polisi.
Kijana huyo amekuwa akiishi Marekani eneo la New Jersey kwa kujificha kwenye gari kwa zaidi ya miezi 18 na kuna ripoti kuwa amekuwa akisumbuliwa na kichaa.
Maofisa wa polisi walisema, mipango yake ilishindwa kutekelezeka kutokana na umakini wa vikosi vya ulinzi vya usalama ambavyo viliwajibika haraka kudhibiti tukio lolote ovu.
Mgombea huyo wa urais amekuwa akishutumiwa na makundi mbalimbali ya watu kutokana na misimamo yake na hivi karibuni, Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden alimlaumu kwa kauli zake ni za hatari.
Katika hatua nyingine, Trump amemfukuza kazi meneja kampeni wake Corey Lewandowski, kwa maelezo kuwa amekuwa na uhusiano mbaya na baadhi ya watendaji kwenye timu hiyo ya kampeni.
“Lewandowski hatafanya kazi nasi tena kwenye kampeni,” alisikika akisema msemaji wa kampeni Hope Hicks.
Hata hivyo, Hicks alitoa shukrani kwa kazi nzuri ya Lewarndowski kwa kipindi alichokuwa nao.
Lewandowski ambaye alifanya kazi na Trump tangu Juni mwaka jana, alilezewa na wachambuzi wa siasa kama mtu mwenye uhusiano mbaya na waandishi wa habari na pia baadhi ya maofisa wa chama cha Republican.
Kwa hivi sasa, kura za maoni za Trump zimekuwa zikishuka na amekuwa akipambana na watu wanaompinga ndani ya Republican ambao wana wasiwasi kuhusu kauli zake za utatanishi.
Trump anaendelea kuzunguka katika maeneo mbalimbali kunadi sera zake, huku akisubiri kuidhinishwa rasmi na chama chake katika mkutano mkuu uliopangwa kufanyika mwezi ujao.
Katika siku za hivi karibuni mikutano ya bilionea huyo imekuwa ikikumbwa na dosari kutokana na kuingiliwa na makundi ya watu wanaopinga misimamo yake.
Hivi karibuni alilazimika kusitisha baadhi ya mikutano hiyo baada ya waandamanaji kujitokeza kwa wingi na kuwasababisha maofisa usalama kuingiwa na wasiwasi.
Kuna uwezekano mkubwa katika uchaguzi ujao, Trump akapambana na Hillary Clinton aliyeshinda kura za mchujo katika Chama cha Democratic.
Wamarekani wanatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu Novemba mwaka huu.