» » Hatima ya Lugumi mikononi mwa Spika

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dodoma. Hatima ya ripoti ya Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa kufunga vifaa vya utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi, ipo mikononi mwa Spika wa Bunge.

Akizungumza bungeni jana, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo iliyoundwa kufuatilia sakata hilo, Japhet Hasunga alisema bado ripoti hiyo ipo mikononi mwao kwa ajili ya marekebisho.

“Bado tunaifanyia marekebisho ili iendane na hadidu za rejea tulizopewa, baada ya hapo tutaipeleka kwenye kamati na wao baada ya kuridhia wataipeleka kwa Spika,” alisema.

Hasunga ambaye pia ni mbunge huyo wa Vwawa (CCM), alisema uamuzi wa kama taarifa ipelekwe bungeni utakuwa wa Spika.

Alisema kabla ya kumalizika kwa mkutano wa bajeti unaoendelea ripoti hiyo itakuwa tayari.

Kamati ndogo iliundwa kutoka Kamati ya Hesabu za Serikali, (PAC) ili kuchunguza sakata hilo na kuandika ripoti kwa kamati.

Mbunge huyo alisema kamati ilipewa kazi ya kuchunguza undani wa mkataba huo wenye thamani ya Sh37 bilioni Aprili 23, mwaka huu.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post