Dar
es Salaam. Raia wa China wameelezwa kuongoza kuingia nchini kinyume cha
sheria katika kipindi cha miezi minne (Januari mpaka Aprili) wakifuatiwa
na Waethiopia.
Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka,
Wilson Bambaganya alitoa taarifa hiyo jana katika mkutano na wanahabari
akisema jumla ya wahamiaji haramu 4,792 wamekamatwa nchini katika
kipindi hicho.
“Serikali
inaandaa mikakati ya kudhibiti na kutambua njia zote za panya (zisizo
rasmi) ambazo hutumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini kinyume cha
sheria ili kudhibiti tatizo hilo.
Alisema
changamoto kubwa katika udhibiti wa wahamiaji haramu ni ukubwa na uwazi
wa mipaka yetu sanjari na uwanda mkubwa wa bahari.
“Serikali
inafanya jitihada kubwa kuhakikisha tatizo hili linadhibitiwa licha ya
kuwapo kwa magari machache ya doria hususani maeneo ya mipakani na boti
lakini jitihada zinafanyika kutatua,” alisema Bambaganya.
Kaimu
Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na Fedha ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa
Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya alisema operesheni ya kuwaondoa
wahamiaji haramu nchini imefanikisha kubaini waliokamtwa.
“Wahamiaji
388 walikamatwa na kulipa faini, 509 upelelezi wao bado unaendelea
ikiwa ni pamoja na taratibu za kimahakama na kujenga ushahidi,” alisema.