Aliyasema hayo alipokuwa akichangia hoja katika semina ya kuwajengea uwezo wabunge wa kupambana na ufisadi iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi (ACFE).
Alidai kuna mbunge aliyekuwapo kwenye bunge lililopita, alikuwa miongoni mwa waliopokea fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, lakini hakuwahi kuhojiwa na Takukuru wala kuzungumziwa hadi sasa.
Profesa Tibaijuka alisema kitendo hicho kinaonyesha ni kwa namna gani Takukuru hawako makini.
