» » RC Tabora apiga marufuku kuuza chakula nje

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amepiga marufuku wananchi kuuza mazao na wafanyabiashara kununua na kuyasafirisha nje ili kukabiliana na janga la njaa linaloweza kujitokeza siku za usoni.

Agizo hilo limetolewa jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Urambo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwananchi Square wilayani humo.

Mwanri alisema kuwa kama mkoa wa Tabora ukipata mvua za kutosha hautakuwa na upungufu wowote wa chakula ila akatahadharisha kuwa jitahada za makusudi za kutunza chakula ni lazima zichukuliwe ili kuzuia mianya yoyote ya kuuza chakula kiholela.

Alisema wananchi wamepata chakula cha kutosha na ni wajibu wao kila mmoja kuhakikisha anajiwekea akiba ya kutosha ili kumaliza msimu vizuri na kuingia msimu mwingine sambamba na kuacha utegemezi serikalini.

Hata hivyo alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Queen Mlozi, kusimamia vyema na kuhakikisha chakula kilichopo wilayani humo hakiuzwi nje ikiwa ni pamoja kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara watakaobainika kujihusisha na utoroshaji wa chakula.

Alimtaka Mkuu wa Wilaya hiyo ahakikishe magari yote ya mizigo yanayoingia na kutoka katika wilaya yake yanakaguliwa na ukaguzi ufanywe chini ya maofisa wa Polisi kwa umakini.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post