» » Rushwa, woga vyatajwa kukwamisha wanawake

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


RUSHWA ya ngono, woga na mfumo dume vimetajwa kuendelea kuzorotesha maendeleo ya wanawake na wasichana wanaotaka kushika madaraka ya uongozi ndani ya jamii.

Hayo yalibainishwa jana na wanawake na wasichana waliohudhuria Semina ya Mafunzo kwa wasichana na wanawake katika kukuza haki zao kwenye nyanja ya kisiasa na uongozi yaliyoandaliwa na Shirika la Wanahabari la Elimisha kwa ufadhili wa Woman Fund Tanzania (WFT).

Walisema licha ya wanawake na wasichana kuanza kuhamasika kuwania nafasi za uongozi kupitia vyama vya kisiasa, bado kuna vizuizi vya kutaka kuyafikia malengo yao.

Walisema bado wapo baadhi ya wanajamii wanaoamini mwanamke hawezi kuongoza, wapo wanaotaka kutumia fursa za kuwapitisha wanawake kugombea uongozi wajinufaishe kwa kufanya nao ngono na pia wapo baadhi ya wanawake wanaoshindwa kuthubutu kuwania nafasi za uongozi kutokana na woga.

Mmoja wa washiriki hao, Tumaini Luhanga alisema vikwazo hivyo havipaswi kuwakatisha tamaa wanawake na wasichana kwa kuwa anaamini kupitia mafunzo mbalimbali makundi hayo yatazidi kubadilika na kupaza sauti ya ukombozi.

Juliana Ndalap, alisema kampeni ya kuwainua wanawake inapaswa kuanzia ndani ya familia kwa wanafamilia wote kutambua kuwa mwanamke naye ana uwezo wa kuwa kiongozi ndani ya jamii kama ilivyo kwa mwanamume.

Mkurugenzi wa Shirika la Elimisha, Festo Sikagonamo aliwataka wanawake na wasichana kutokatishwa tamaa na vikwazo vilivyopo badala yake waanze kujijengea msingi mzuri wa uongozi kupitia vikundi vidogo vidogo vilivyopo kwenye jamii zao.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post