ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Leo polisi wamevamia kwenye nyumba ya msanii wa filamu
bongo, Faiza Ally kwa kufanya uchunguzi kutokana na taarifa walizozipata
kuwa msanii huyo ni muuzaji wa madawa ya kulevya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliandika:
Leo tarehe 3/June/2016 Kwa Kweli ni siku ambayo sitakuja
kuisahau kwenye maisha yangu-wamekuja maaskari saba kwangu wakiwa na
silaha!!! Eti wamepata taarifa eti mimi nabeba madawa ya kulevya kweli?
MANGE kila siku anawataja wahusika lkn sijui Kama wanafatiliwa leo
nafatiliwa mtu kama mimi ambaye sijawahi wala kuwaza nifanye hivyo?
Kweli mtu unatoka kwako kwenda kutoa taarifa za uongo bila kuwa na
uhakika wala uthibitisho wowote! Kwa Kweli nimewanyanyulia mikono
walimwengu

ila nimesikitishwa sana Kwa yoyote alienda kupeleka taarifa hizo police
amekosea sana Na InshaAllah M.Mungu atamuathibu Kwa namna ambayo
anaijua yeye! Mimi sijui walimwengu mnanionaje ? Natamani mnijue nikoje!
LIFE IS NOT FAIR……lkn Kama muonekano wangu Ndio unanifanya nishukiwe
kuwa najihusisha na madawa! Kama ni muonekano wangu unanifanya nionekana
malaya! Kama ni muonekano wangu unanifanya nikashifiwe Basi wallah
sitabadilika Kwa kuwa naamini M.Mungu ameniumba hivi Kwa sababu
ntaendelea kuwa mimi siku zote na sintabadilika kamwe Maana MUNGU
HAJAWAHI KUNIANGUSHA HATA SIKU MOJA NA HATA NIANGUSHA KAMWE……… Poleni
sana mliopeleka taarifa za uongo police nimesachiwa kwangu bila hofu
yoyote huku nikiwa nimekabithi maisha yangu mikononi Kwa M.Mungu Japo
nilikua na hofu ya kuwa huenda kuna mtu amenichukia labda anataka kunipa
kesi lkn mwisho wa siku nimekua mshindi Kwa mara nyingine na si kwamba
nina uwezo ila ni Mungu tu na usafi wa moyo wangu ! NARUDIA TENA
NATAMANI WATANZANIA NA ULIMWENGU WANIJUE NIKOJE – LKN NAKUBALI TENA KWA
MARA NYINGINE LIFE IS NOT FAIR…….

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO