» » » Amissi Tambwe Aishauri Yanga

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameushauri uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unasajili kiungo mkabaji (namba sita), wa nguvu katika kipindi hiki cha usajili ambaye atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo.

Tambwe ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao 21, amesema Yanga inakabiliwa na tatizo kubwa la kiungo mkabaji mwenye uwezo kupambana muda wote wa mchezo.

Alisema hali hiyo ndiyo imekuwa ikiisumbua timu hiyo katika mechi zake za kimataifa jambo ambalo uongozi wa timu hiyo unapaswa kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili.

“Tuna viungo wengi wazuri lakini bado tunahitaji kiungo mkabaji wa nguvu ambaye atakuwa anashirikiana vilivyo na mabeki wetu katika safu ya ulinzi.

“Uongozi wetu unatakiwa kuliona hilo na kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili kabla ya kuanza kushiriki michuano ya kimataifa ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya timu tutakazokutana nazo,” alisema Tambwe.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post