
Dodoma.
Wito umetolewa kwa marais na maspika wastaafu wa Tanzania kusaidia
kutoa ushauri wa namna bora ya uendeshaji wa shughuli za vikao vya Bunge
kwa sasa, hususani katika kipindi hiki cha vyama vingi ili wananchi
waweze kuwakilishwa vyema zaidi kuhusu mahitaji yao bungeni.
Pia,
Watanzania wametakiwa kufanya maombi maalumu yenye lengo la kuliombea
Bunge ili liweze kurudi katika misingi ya awali kwa kujenga umoja,
mshikamano na uvumilivu wakati wa vikao na kuweka mbele dhamira ya ya
kuwawakilisha wananchi.
Wito
huo umetolewa na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mt Paulo wa Msalaba la
mjini Dodoma, Padri Sebastian Mwaja wakati wa mahubiri ya ibada
iliyofanyika kanisani hapo.
“Bunge
la sasa linaloendelea na vikao vyake hapa Dodoma linawanyong’onyesha
wengi kwa kushindwa kujikita katika taratibu na desturi nzuri za
Kitanzania za kujenga umoja, mshikamano na kuvumiliana katika mambo yetu
mbalimbali,”amesema Padre Mwaja.
