
Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi, Vijana
na Walemavu, Jenista Mhagama amewataka wafanyakazi wa majumbani
kutoshirikiana na wauaji wanaovizia kuwatoa uhai waajiri wao.
Mhagama ametoa kauli hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi wa majumbani kimataifa yaliyofanyika kitaifa mjini Dodoma.
Amesema
kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wamekuwa chanzo cha mauaji ya waajiri
wao kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana na wauaji katika kuyatekeleza.
“Nataka
niwaambie jambo moja, mnapokuwa mnafanya kazi hakikisheni kuwa
mnazingatia kanuni na sheria za ajira ambazo zinawalinda na siyo kwenda
kuiba, kuua au kushirikiana na wauaji katika kuwaua waajiri wenu,”
amesema Mhagama.
