
Shinyanga.
Jeshi la polisi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga linamshikilia mtu
mmoja mkazi wa kijiji cha Masagala kata ya Maganzo wilayani Kishapu, kwa
kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka mitatu na kumsababishia maumivu
makali sehemu za siri.
Mkuu
wa kituo cha polisi Magazo, Osca Shani alisema tukio hilo lilitokea
Juni 7, mwaka huu na kwamba baada ya mtoto kufikishwa kwenye kituo cha
afya alibainika kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili.
“Tunamshikilia
mtuhumiwa kwa kosa la kubaka na kumsababisha maumivu makali mtoto wake
na kamba atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka,” alisema Shani.
Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu, Hawa Ng’humbi alivitaka vyombo vya dola
kutoichezea kesi hiyo na kwamba mtuhumiwa afikishwe mahakamani hata na
kufungwa jela ili kuondoa matatizo ya ubakaji kwenye wilaya hiyo.
