Kampuni
ya kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya
habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya
kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika.
Hata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban
saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa!
Amini usiamini, KENGEN imempata nyani
mmoja katika eneo maalum lenye ‘swichi’ hiyo katika mtambo wa kuzalisha
umeme ulioko kwenye bwawa kuu la Gitaru Mashariki mwa Kenya.
Sasa kampuni hiyo inasema huenda nyani huyo ndiye aliyezima umeme kote nchini Kenya !
Kengen inasema kuwa huenda nyani huyo
aliangukia mashine hiyo ndogo na ”kusababisha hitilafu ya takriban
megawati 180 za umeme ambao ndio uliosababisha ukosefu wa umeme kote
nchini Kenya.”
Kwa takriban saa nne taarifa hiyo ilielezea.
Tumbili huyo alinusurika na sasa amechukuliwa na shirika la huduma kwa wanyama pori KWS ilikupokea matibabu.
“mitambo ya kuzalisha umeme kote nchini
Kenya huwa imezingirwa na nyaya za umeme ilikuwazuia wanyama wa porini
kuingia humo na kusababisha madhara kama hayo ya jana , taarifa hiyo
ilisema.
”Tunaomba radhi kwa tukio hilo la
kipekee la hapo jana na sasa tumeanza kuweka mikakati dhabiti ya kuzuia
marudioa ya ajali hiyo” taarifa hiyo ya KenGen ilielezea.
Mashirika mengi pamoja na wawekezaji wa
kibinafsi walilazimika kufunga biashara zao hapo jana huku wale
waliokuwa na nitambo binafsi za kuzalisha umeme wakiingia gharama zaidi
ya kununua mafuta .
Wakenya wengi waliopokea habari hizo waliikejeli kampuni hiyo ya kuzalisha umeme wengi wakiwatania katika mitandao ya kijamii.