» » Msalala wakaribia kushinda vita dhidi ya madawati

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Kahama. Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imefanikiwa kutengeneza madawati 4,263 kati ya 4,661 yanayohitajika, hivyo kubaki na upungufu wa madawati 396 kwa shule za msingi.

Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Msalala, Vivian Masangya amesema kati ya madawati hayo yaliyotengenezwa, Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu umechangia 1,380.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa ameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo na kutaka nyingine kujifunza kutoka kwao.

Kawawa amewahimiza kukamilisha idadi ya madawati iliyosalia ili kukwepa rungu la Serikali dhidi ya watendaji watakaoshindwa kabla Juni 30.

“Halmashauri za Ushetu na Mji Kahama, zinapaswa kujifunza kutoka Msalala ili zitimize maelekezo ya Serikali kabla ya Juni 30,”amesema Kawawa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post