Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya sandarusi maarufu ‘Viroba’ cha Bubugao Footwear Co Limited kilichopo Kata ya Tambani wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani, kimelidanganya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kuwa hakijaanza uzalishaji.
Kutokana na hali hiyo kiwanda hicho kimefungiwa na kutozwa faini ya Sh5 milioni.
Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki, Jaffar Chimgege amesema jana kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kufanya ukaguzi na kubaini kuwa kiwanda hicho kimeanza kazi bila kibali cha Nemc.
Akizungumzia uamuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Qiu Huashi amesema: “Haina shida kama sheria inasema mfunge kiwanda mpaka nipate kibali, lazima nifuate sheria siwezi kuidanganya sheria wala Serikali.”