» » Lukuvi atema cheche, viongozi wanywea

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Lushoto. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametaka shamba la kahawa la mlowezi wa Kizungu, kupimwa viwanja vya makazi kwa sababu Lushoto ni Mamlaka ya Mji Mdogo haipaswi kuwa na mashamba makubwa katikati ya mji.

Pia, amepiga marufuku uuzwaji shamba la Chama cha Ushirika cha Usambara, lililopo eneo la Bumbuli wilayani Lushoto, Tanga lenye ukubwa wa eka 455.

Lukuvi alitoa agizo hilo juzi alipokuwa akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba mjini Lushoto.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli, Amir Shehiza alisema wamepokea maagizo ya waziri na watayatekeleza kwa faida ya halmashauri.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post